|
Karibuni
na HNG Homepage ! Maelezo ya msingi Shule
ya Heinrich-Nordhoff-Gesamtschule (HNG) katika mji Wolfsburg ni
Comprehensive School (IGS), yaani shule kwa kila aina ya mwendeleo wa elimu ya
shuleni. Katika shule moja wanafunzi wana nafasi kuhitimu shule baada ya vidati
9, 10 (O-level), 11 ili 13 (A-level). Shule
ya Heinrich-Nordhoff-Gesamtschule ni shule ya miradi ya UNESCO.
Shule
iliyojangwa mwaka 1971 yupo sehemu ya kusini magharibi ya mji Wolfsburg, lakini
wanafunzi hutoka eneo la mji zima na mazingira pia. Hivi sasa (tarehe 2002) wanafunzi
1191 wajifunzwa kwa walimu 91 shuleni
petu. Mikondo sita yapo katika kila kiwango cha madarasa na
vidato. Kama idadi ya wanafunzi wanaotaka kuanza madarasa ya kwanza ingepita
ujazo wa kuwakaribisha shuleni, wanafunzi wale wanapoandikishao wanapigwa kura,
lakini iwepo idadi hasa ya wanafunzi wenye matatizo ya kujifunza na wanafunzi
wenye bidii na kipaji, ili wafundishwe wasaidiane. Wanafunzi wafundishwa katika
shule yetu toka kidati 5 (yaani baada ya shule ya msingi) hadi kidati 10 (O-level).
Kama wangefanikiwa katika masomo yao yote waweza kuendeleza elimu ya shuleni yao
vidati 11, 12 na 13 kabla ya kufanya mtihani wa mwisho (unaohusika mtihano wa
kidato cha 6).
Shule yetu inaongozwa kwa timu ya
wakurugenzi: mwalimu mkuu, makamu wa walimu mkuu, mkurugenzi wa madarasa 5
hadi 10, mkurugenzi wa vidato 11 hadi 13 na kiongozi cha mambo ya ualimu. Kila
kidato kina kiongozi pia na kila darasa huongozwa kwa walimu wa darasa wawili. Shule
ya Heinrich-Nordhoff-Gesamtschule ni shule ya kutwa nzima. Mafunzo huanza
saa mbili kasoro dakika tano asubuhi na humaliza saa kumi kasoro dakika kumi. Hakuna mafunzo alasiri mbili kwa wiki na Jumamosi. Kila
siku tangu saa moja na nusu wanafunzi huweza kununua kula kidogo na vinywaji.
Toka saa nne hadi saa sita huweza kuchagua menyu kadhaa za chakula cha mchana
bwaloni. Katika breki ya adhuhuri wanafunzi wana nafasi kujipumza ili kucheza (kwa
mfano katika sebule ya michezo, katika chumba cha tenisi ya mezani, mkahawani,
chumbani cha Internet na kadhalika). Alasiri bila mafunzo waweza kushikiri
katika shughuli kadhaa, kwa mfano mpira, compyuta, kazi ya mikinoni n.k.. Katika maktaba kubwa ya shule wana nafasi kusoma ili kuazima vitabu,
kujifunza peke yao na kufanya mazoezi pamoja. Masomo ya
wanafunzi katika shule moja Wanafunzi wa kila aina ya kipaji na uelekevu
wanafundishwa katika majengo hasa ya shule yetu madarasani O-level na A-level (Ujerumani
yanayihusika madarasa 5 hadi 10 na vidato 11 hadi 13). Yaani baada ya shule ya
msingi wanafunzi waweza kukaa katika shule yetu ya HNG hadi mtihani wa kidato 6
(Ujerumani ni 'Abitur' baada ya kukimaliza kidato 13). Si lazima waendeleze
elimu ya shuleni katika shule nyingine.
Walimu wanafundisha wanafunzi wa kila darasa kwa
timu inayahusika ya kuwa uhusiano imara wa binafsi baina ya walimu na
wanafunzi wao bila mabadiliko mengi. Malengu
yetu muhimu ya elimu ya shuleni ni kujifunza kwa pamoja na kwa kuunga mkono.
Tutaka kupatanisha furaha ya kujifunza kwa wanafunzi wetu. Kwa hiyo ikiwezekana
hatutaki shauri upesi kuhusu mwenendo wa kila mwanafunzi katika shule yetu na
mtihani wake wa mwisho ili tujiepushe makosa na mwisho wa elimu ya shuleni wa
mapema mno kama mnafunzi ye yote angekuwa na shida. Katika
shule yetu inawezekana kujifunza elimu ya shuleni ya kila aina: -
mwisho baada ya kidato 3 (Ujerumani ni kidato 9) -
mwisho baada ya kidato 4 (Ujerumani ni kidato 10) - mtihani wa O-level - mtihani wa A-level Wanafunzi wa kila kidato
wanafundishwa kwa pamoja katika madarasa yao hasa yanachohusika kidato chao.
Wanamojifunza masomo ya kijerumani, kiingereza, kifaransa, kihispaniola au
kilatini, masomo ya hisabati, masomo ya jamii (yaani geography, history na
civics), masomo ya dini na maadili. Kwa namna hii waweza kupata mwelekeo na hisi
ya uanachama wa kidato chao upesi sana. Masomo machache hayafunzwa madarasani pa
kidato yanachohusika kwa sababu yahitaji madarasa hususa. Haya ni michezo,
masomo ya compyuta, masomo ya ufundi, masomo ya muziki na sanaa. Shuleni wanafunzi wana nafasi nyingi kwa michezo, kwa mapumzika na kula (bwalo
kubwa na vioski viwili vya kula kidogo) na juu ya hiyo kwa kujifunza peke yao (kwa
mfano katika maktaba kubwa ya shule). Mafunzo ya kiswahili Toka mwaka 1999 wanafunzi wa shule
yetu wana nafasi kujifunza luhga ya Kiswahili mara moja kwa wiki. Kiswahili ni
lugha ya Afrika ya Mashariki na sehemu kadhaa ya Afrika ya Kati. Hususan ni
lugha ya Tanzania, yaani nchi ya washirika wetu wa ushirikiano wa shule.
Mafunzo ya Kiswahili si kawaida kwa
shule Ujerumani. Wanafunzi wajivutiao lugha ya Kiswahili wanatoka madarasani 10
hadi 13 (yaani vidato vya O-level na A-level) na wanajifunza kwa hiari katika
darasa moja. Hamu yao ya kufahamu lugha ya Kiswahili inasababishwa kwa kuvutiwa
kwa Wafrika, kwa nchi Tanzania na kwa mila na desturi ya Kiafrika. Wanafunzi
kadhaa wanataka kusafiri Afrika wakati ujao ili wamekwisha kufanya safari katika
nchi ya rafiki yetu wa Kiafrika. Wote wajua kwamba Kiswahili inaenea
katika Afrika na kwa hiyo ni lugha muhimu sana kwa mawasiliano na uchumi. Lakini lugha ni
ngumu kiasi kwa wanafunzi wa Kijerumani kwa sababu inatofautiana sana na lugha
za Ulaya. Kwa hiyo wanafunzi wetu wajifunza Kiswahili kwa michezo bila alama na
mitihani ili waweze kufahamu sentensi rahisi na kuongea kidogo. |